Wakati umefika sasa kwa
polisi wa usalama barabarani Jijini Dar es salaam wakishirikiana na wadau
wengine kukemea kwa nguvu kero ya vyombo vya moto hasa pikipiki na magari
ambapo madereva wake wamekuwa wakilazimisha kupita sehemu maalumu ambazo zimetengenezwa
kwaajili ya watembea kwa miguu.
Jambo hili limekuwa likitishia uhai wa watembea
kwa miguu jijini Dar es salaam ambao mara nyingi wamekuwa wakipata misukosuko
ya hapa na pale ya kunusulika kugongwa na
magari na pikipiki hasa inapofika majira ya jioni ambapo wengi huwa wamejikita hasa katika matumizi ya simu zao za mkononi huku wengine wakiwa na pilikapilika za kuwahi usafiri.
Hatuna budi kuwajuza
madereva wote ambao wamekuwa na haraka ya kufika makwao zaidi yaw engine yakuwa
zile barabara zimetengenezwa kwaajili ya watembea kwa miguu tu, kwahiyo ni
lazima waheshimu sheria na taratibu za barabarani.
Nina imani ya kuwa
serikali iliona ipo haja ya kuwatengenezea wananchi wake semu zao maalumu za
kutembelea. Sasa ni kivipi madereva wale wasiojiheshimu wanadhubutu kupuuza agizo ilo la serikali?
Hakika mazoea haya sio
mazuri hata kidogo kwa sababu tabia hii itaota mizizi ambayo itakomaa huku
wananchi wakiendelea kukumbwa na vifo pamoja na ulemavu unaosababishwa na
baadhi ya madereva wazembe.
Hili sio suala la polisi
wa usalama pekee bali ni la watu wote wapenda maendeleo na mabadiliko, lakini
ni muhimu kwa vyombo vya dola kuweka sheria madhubuti zitakazoweza kuwabana
madereva wanaovunja sheria na kukabiliana nazo kwa wakati sahihi.


No comments:
Post a Comment