Licha yakuwa na sifa kedekede Jiji la Dar es salaam limeendelea kuwa chafu kila kukicha kutokana na baadhi ya wakazi kutojua umuhimu wa kutunza mazingira.
kutokana na kutokujua kwao kumepelekea karibu kila kona ya jiji hili kuwa na harufu mbaya iliyotapakaa kila mahali.
Baadhi ya wakazi hasa waishio maeneo ya uswahilini wamegeuza vituo vya Daladala kuwa kama sehemu maalumu za kuweka uchafu, cha kushangaza ni kuwa mara kadhaa wamekuwa wakitupa mchana kweupe bila ya kuchukuliwa hatua yoyote.
Ni bora taka hizo zingekuwa zakawaida lakini cha ajabu wengine wanathubutu kutupa kinyesi pamoja na mikojo iliyowekwa kwenye chupa za maji safi.
Wengine wamejiwekea ratiba ya kutupa taka zao sehemu zisizo rasmi, mara nyingi utawaona muda wa usiku na mapema asubuhi wakiwa wamebeba mafurushi makubwa utafikiri wasafiri, kumbe wanatafuta sehemu za kutupa taka zao.
Kutokana na kutapakaa kwa taka hizo kumepelekea milipuko ya magonjwa mbalimbali hasa kipindi cha mvua magonjwa kama kipindupindu, kichocho na taifodi yamekuwa yakiwaadhili hasa watoto wadogo.







