![]() |
| Askari wa jeshi la kutuliza gasia wakikabiliana na wakulima |
Umepita muda sasa
mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha laitimi mkoani Dodoma
bado hauja tafutiwa ufumbuzi huku baadhi ya wakulima na wafugaji wakiripotiwa
kuuwawa.
Kila jamii imekuwa
ikidai kuwa wao ndio wamiliki halali wa eneo hilo ambalo limekuwa likiwaingiza
katika mgogoro mkubwa kila mwaka hasa ifikapo kipindi cha masika na kiangazi,
ambapo kwa muda huo wakulima wanakuwa katika uzalishaji na mavuno huku wafugaji
wakitafuta maeneo ya malisho kwaajili ya mifugo yao.
Kutokana na sintofahamu
hiyo kuhusu ni nani mmiliki halali wa eneo hilo kati ya wakulima ambao ni jamii
ya wagogo na wabena dhidi ya wafugaji jamii ya wamasai wengi wao wakitokea
mikoa ya kaskazini yaani manyara na kiteto, hivyo basi kila jamii inajiona
inamamlaka zaidi kuliko mwenzake.
Kwakuwa mgogoro huu
bado haujapata utatuzi wa kudumu machafuko yamekuwa yakiendelea kila kukicha
huku jamii kubwa inayo adhilika ni wakulima hasa kabila la wagogo, vifo hivyo
vimekuwa vikitokea hasa kwa kabila la wagogo kwasababu mara nyingi wamekuwa
vibarua walioajiliwa na watu wa jamii ya wabena hivyo katika kipindi chote cha
kilimo huishi katika mashamba.
Jitihada kubwa Zimekuwa
Zikifanywa na vingozi mbalimbali wakijaribu kutatua mgogoro huu akiwemo mbunge
wa Dodoma mh. Jobu ndugai, japokuwa jitihada zake bado hazijaonesha mafanikio
yoyote hadi sasa.
Mgogoro huu sio wa
Ndugai peke yake au wakulima na wafugaji wa mkoa wa Dodoma tu, yatupasa jamii
yote ya watanzania kushirikiana kwanguvu ili kushuluhisha mgogoro huu kama si
kuumaliza kabisa kwakuwa hakuna kisicho wezekana endapo tutawekania dhabiti
katika jamobo hili.
![]() |
| Wakulima wakichangia jambo ka |


No comments:
Post a Comment