Ni muda mrefu umepita
baada ya mamlaka yainayoshughulika na usafiri wan chi kavu na majini SUMATRA,
walipotoa amri ya kupiga marufuku wapigadebe wa kituo cha mabasi yaendayo
mikoani na nchi jirani cha Ubungo,wasiokua na sare kuwasumbua abiria.
Kwa kipindi kifupi tu
tatizo hilo lilikomeshwa kwa kutumia nguvu za ziada na hatimae wakawaondoa wapigadebe wote waliokuwawanafanya kazi kiholela na hatimae usumbufu ulipungua.
Kutokana na kutokuwepo
kwa mipango endelevu hali ile ya mwanzo imejirudia tena, ila sasa inatisha
kwani wapigadebe wamekuwa wengi mno kiasi kwamba hata wale wenye sare
hawaonekani.
Kitu cha ajabu zaidi wapigadebe wasiovaa sare ndio wamekuwa kipaombele kwa kuwapokea wabiria na
kuwapeleka ofisi za mabasi husika kwa nia ya kukata tikiti. Hali hii imepelekea
kwa wale abiria wageni wa jiji la Dar es salaam, kulizwa kila kukicha ambapo
wamekuwa wakitapeliwa mizigo yao
pamoja na vitu vingine vidogo vidogo kama nauli na simu za mikononi.
Kwa kuwa mpango huu
ulianza kwa malengo dhabiti Sumatra hawanabudi kujipanga tena upya kwaajili ya
kuikomesha kero hii ambayo imekuwa ikitoa picha chafu kwa wageni wanaofika
jijini Dar es salaa.






