Pages

Friday, 24 October 2014

USUMBUFU WA WAPIGADEBE UBUNGO BADO NI KERO.



Ni muda mrefu umepita baada ya mamlaka yainayoshughulika na usafiri wan chi kavu na majini SUMATRA, walipotoa amri ya kupiga marufuku wapigadebe wa kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo,wasiokua na sare kuwasumbua abiria.



                



Kwa kipindi kifupi tu tatizo hilo lilikomeshwa kwa kutumia nguvu za ziada na hatimae wakawaondoa wapigadebe wote waliokuwawanafanya kazi kiholela  na hatimae usumbufu ulipungua.

Kutokana na kutokuwepo kwa mipango endelevu hali ile ya mwanzo imejirudia tena, ila sasa inatisha kwani wapigadebe wamekuwa wengi mno kiasi kwamba hata wale wenye sare hawaonekani.




                 



Kitu cha ajabu zaidi wapigadebe wasiovaa sare ndio wamekuwa kipaombele kwa kuwapokea wabiria na kuwapeleka ofisi za mabasi husika kwa nia ya kukata tikiti. Hali hii imepelekea kwa wale abiria wageni wa jiji la Dar es salaam, kulizwa kila kukicha  ambapo  wamekuwa wakitapeliwa mizigo yao  pamoja na vitu vingine vidogo vidogo kama nauli na simu za mikononi.
 

Kwa kuwa mpango huu ulianza kwa malengo dhabiti Sumatra hawanabudi kujipanga tena upya kwaajili ya kuikomesha kero hii ambayo imekuwa ikitoa picha chafu kwa wageni wanaofika jijini Dar es salaa.


Tuesday, 21 October 2014

SERIKARI IMESHINDWA KUZUIA ONGEZEKO LA GEREJI BUBU?


Kumekuwa na malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na wakazi wa jiji la Dar es salaam, juu ya wingi wa sehemu za kutengenezea vyombo yva usafiri maarufu kama Gereji bubu           kuwepo kwa kila mtaa.









Hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wanao ishi kando kando mwa gereji hizo, ambao wamekuwa wakikerwa hasa na kelele zinazotokana na mashine wanazozitumia mafundi wakati wa ukataji wa vyuma pamoja na kauli chafu za baadhi ya mafundi.

Kutokana na kuongezeka kwa gereji hizo zisizo rasmi kunatishia usalama wa raia waishio karibu na maeneo hayo, kwa sababu inaweza kutokea mlipuko wowote utakao sababishwa na mafuta ya petrol au disel.

Ijapokuwa serikari imekuwa ikijitahidi katika hili na kuzifungia baadhi ya gereji bubu, lakini bado baadhi ya watu wameendelea kufungua kiholela bila ya kujali eneo pamoja na usalama wa wakazi wa karibu na maeneo husika.


Thursday, 9 October 2014

MALUMBANO SIO SULUHISHO SAHIHI LA MIGOGORO.



Umefika wakati wakujiuliza ni lini hasa malumbano na migogoro ya wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kwa jina la wamachinga na uongozi wa jiji la Dar es salaamambao haujapatiwa ufumbuzi hadi leo.








Kila upande umekuwa ukitoa sababu zake tena zakueleweka, lakini bado haujifikiwa muafaka mzuri juu ya mgogoro huo. Kwa upande wa serikali wamekuwa wakijitetea kuwa wameshawatengea maeneo maalumu ya kufanyia biashara mfano mzuri ni lile jengo lililopo ilala la MACHINGA COMPLEX.

Kwa upande mwingine wafanyabiashara wadogowadogo wamekuwa wakiilalamika kuwa serikali imekuwa ikiwatoza kiwango kikubwa katika vitalu na pia maeneo waliyotengewa hayana mvuto kwa wateja.

Kutokana na kutofikiwa kwa muafaka wa mgogoro huo kumepelekea kutapakaa kwa wamachinga sehemu mbalimbali ndani ja jiji la Dar es salaam kama Manzese, Kariakoo na Ubungo.






 
Serikali kwa kushirkiana na wamachinga haina budi kukaa chini na kutafuta suluhisho la mgogoro huu, kwa kuwa mgogoro huu sio wa Dar es salaam peke yake bali ni kero karibia Tanzania nzima mikoa kama ya mwanza na mbeya migogoro hii imekuwa ikiibuka kila wakati.
 
Kiasi kwamba wamachinga wamekuwa wakivamia maeneo yasiyo rasmi na kusababisha ufinyu wa maeneo kama vile barabara na vituo vikuu vya kapakia na kushushia abiria

Monday, 6 October 2014

HATUNA BUDI KUWAJIBIKA KATIKA HILI.



Wakati umefika sasa kwa polisi wa usalama barabarani Jijini Dar es salaam wakishirikiana na wadau wengine kukemea kwa nguvu kero ya vyombo vya moto hasa pikipiki na magari ambapo madereva wake wamekuwa wakilazimisha kupita sehemu maalumu ambazo zimetengenezwa kwaajili ya watembea kwa miguu. 








 Jambo hili limekuwa likitishia uhai wa watembea kwa miguu jijini Dar es salaam ambao mara nyingi wamekuwa wakipata misukosuko ya hapa na pale ya  kunusulika kugongwa na magari na pikipiki hasa inapofika majira ya jioni ambapo wengi huwa wamejikita hasa katika matumizi ya  simu zao za mkononi huku wengine wakiwa na pilikapilika za kuwahi usafiri.

Hatuna budi kuwajuza madereva wote ambao wamekuwa na haraka ya kufika makwao zaidi yaw engine yakuwa zile barabara zimetengenezwa kwaajili ya watembea kwa miguu tu, kwahiyo ni lazima waheshimu sheria na taratibu za barabarani.

Nina imani ya kuwa serikali iliona ipo haja ya kuwatengenezea wananchi wake semu zao maalumu za kutembelea. Sasa ni kivipi madereva wale wasiojiheshimu  wanadhubutu kupuuza agizo ilo la serikali?









Hakika mazoea haya sio mazuri hata kidogo kwa sababu tabia hii itaota mizizi ambayo itakomaa huku wananchi wakiendelea kukumbwa na vifo pamoja na ulemavu unaosababishwa na baadhi ya  madereva  wazembe.

Hili sio suala la polisi wa usalama pekee bali ni la watu wote wapenda maendeleo na mabadiliko, lakini ni muhimu kwa vyombo vya dola kuweka sheria madhubuti zitakazoweza kuwabana madereva wanaovunja sheria na kukabiliana nazo kwa wakati sahihi.




Wednesday, 1 October 2014

MADEREVA BODABODA WAPEWE ELIMU YA USALAMA.

Madereva wa pikipiki (Bodaboda) jijini Dar es salaam wanatajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara na kupelekea vifo au ulemavu kwa uzembe uliopitiliza.









Asilimia kubwa ya madereva hao wamekua wakiendesha pikipiki kwa mwendo kasi mno bila ya kujali usalama wao wala watembea kwa miguu.

Sheria zimekuwa zikifunjwa tena kwa makusudi kiasi kwamba madereva hao, hawakupitia shule ijapokuwa sheria pamoja na askari wa usalama barabarani kuweka mkazo katika utekelezwaji huo wa sheria, kama vile kuvaa kofia ngumu kichwani ambapo madereva wengi wamekuwa hawatii amri matokeo yake hupoteza maisha mara tu baada ya kupata ajali.







Lakini sio jambo la ajabu kwa madereva kuvunja sheria hizo, kwa kuwa kunabaadhi ya madereva wameletewa leseni za udereva majumbani mwao huku wengine hawana kabisa vigezo na hata hizo leseni hawajui zipo katika muundo gani.

Huu ni ushauri wa bure kwa maderea na wanajamii kwa ujumla yatupasa kutambua kuwa mabadiliko yanaanzia kwako.



Tuesday, 30 September 2014

HILI NALO LINAHITAJI ELIMU?

Licha yakuwa na sifa kedekede Jiji la Dar es salaam limeendelea kuwa chafu kila kukicha kutokana na baadhi ya wakazi kutojua umuhimu wa kutunza mazingira.







kutokana na kutokujua kwao kumepelekea karibu kila kona  ya jiji hili kuwa na harufu mbaya iliyotapakaa kila mahali.

Baadhi ya wakazi hasa waishio maeneo ya uswahilini wamegeuza vituo vya Daladala kuwa kama sehemu maalumu za kuweka uchafu, cha kushangaza ni kuwa mara kadhaa wamekuwa wakitupa mchana kweupe bila ya kuchukuliwa hatua yoyote.

 Ni bora taka hizo zingekuwa zakawaida lakini cha ajabu wengine wanathubutu kutupa kinyesi pamoja na mikojo iliyowekwa kwenye chupa za maji safi.



    






                               

                                                                

Wengine wamejiwekea ratiba ya kutupa taka zao sehemu zisizo rasmi, mara nyingi utawaona muda wa usiku na mapema asubuhi wakiwa wamebeba mafurushi makubwa utafikiri wasafiri, kumbe wanatafuta sehemu za kutupa taka zao.

Kutokana na kutapakaa kwa taka hizo kumepelekea milipuko ya magonjwa mbalimbali hasa kipindi cha mvua magonjwa kama kipindupindu, kichocho na taifodi yamekuwa yakiwaadhili hasa watoto wadogo.  

Monday, 29 September 2014

MAEGESHO YA MAAGARI NI TATIZO MJINI.



Kutokana na kutokuwepo kwa mpangilio mzuri wa maegesho ya magari (PARKING) pamoja na pikipiki jijini Dar es Salaam, kumepelekea tishio kubwa kwa watembea kwa miguu kukumbana na ajali katika nyakati tofauti.



Moja ya sehemu za kuegeshea magari katika mitaa ya kariakoo
                                              


 Kuanzia mazingira pamoja na ufinyu wa maegesho hayo ambayo siyo rafiki kabisa na wakazi wa jiji hili, ambao mara zote wamekuwa na pilikapilika za hapa na pale kwaajili ya kujiingizia kipato chao cha kila siku.

kuna maswali mengi yakujiuliza juu ya wahusika hasa serikali ambayo imekuwa muhusika katika mpangilio wa makazi ya watu pamoja na miundo mbinu kama ya Barabara, mosi kama walijua wafanyakazi wa mjini karibia wote wanamiliki vyombo vya usafiri, kwanini hawakuandaa sehemu maalumu za kuegeshea magari yao? Pili sheria za mipango
miji na zile za barabarani zinaruhusu uegeshaji wa magari kwa vipimo vipi?

Binafsi makazi yoyote yale inabidi yawe umbali wa mita 100, ambayo ndiyo hifadhi ya barabara. Je kwa ukaribu ule wa maegesho ya mitaa ya kariakoo na sehemu nyingine hapa mjini ni mita 100?

Friday, 26 September 2014

YOUNG DEE, APATA SHAVU JIPYA.




Msanii Young Dee a.k.a paka rapper ambaye anafanya vizuri katika muziki wa rap mpaka sasa, ameingia mkataba mnono na kampuni ya Star Times inayojishughulisha na uuzaji wa ving'amuzi kuwa balozi wa channel ya Qyou hapa nchini.

Young Dee ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya unaoitwa "SIO MCHOYO" aliomshirikisha mkali wa R&B bongo Jux a.k.a V tone amekaririwa na Bongo5 kuwa, Star Times wamemlipa kile alicho staili na ndio maana amekubali kusaini mkataba huo.



Young Dee kwa nyuma akiwa ameshika makata



"Nimesaini mkataba na Star Times kutumia picha yangu na pia kama balozi wa Qyou channel ya vijana, kuhusu kunilipa ni jambo langu binafsi ila jua inanilipa vizuri  ndio maana nimekubali kufanya kazi hiyo". Amesema Young Dee.

Thursday, 25 September 2014

MASHABIKI WAMSUBIRI KWA HAMU SUAREZ.

Mshambuliaji machachari anayekipiga katika miamba wa hispania Barcelona FC, Luis Suarez anasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa timu ya Barcelona wakimuona akitandaza kabumbu dimbani hivi karibuni. habari zaidi click HAPA.
LUIS SUAREZ.

Wednesday, 24 September 2014

YOUNG KILLER "NINAFURAHA KUSHIRIKISHWA NA MKONGWE."

kijana mdogo anayefanya vizuri kwa sasa nchini tanzania katika muziki wa hip hop Young killer a.k.a msodoki the son, amesema ana furaha sana baada ya  kushirikishwa na mkongwe aliyekulia katika familia ya muziki banana zoro.
Young killer, Zahir na Banana
katikati ya mwaka huu young killer aliachia wimbo wake mpya "umebadilika" alio mshirikisha mkongwe huyo hivyo basi kutokana na kupokelewa vizuri kwa wimbo huo Banana aliamua kumshirikisha katika wimbo wake huo mpya "samehe sahau" uliotengenezwa katika studio za Dully Syles, 4,12. kwa undani zaidi click HAPA.

Tuesday, 23 September 2014

MIGOGORO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI INAHITAJI SULUHISHO LA KUDUMU.


Askari wa jeshi la kutuliza gasia wakikabiliana na wakulima

Umepita muda sasa mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha laitimi mkoani Dodoma bado hauja tafutiwa ufumbuzi huku baadhi ya wakulima na wafugaji wakiripotiwa kuuwawa.

Kila jamii imekuwa ikidai kuwa wao ndio wamiliki halali wa eneo hilo ambalo limekuwa likiwaingiza katika mgogoro mkubwa kila mwaka hasa ifikapo kipindi cha masika na kiangazi, ambapo kwa muda huo wakulima wanakuwa katika uzalishaji na mavuno huku wafugaji wakitafuta maeneo ya malisho kwaajili ya mifugo yao.

Kutokana na sintofahamu hiyo kuhusu ni nani mmiliki halali wa eneo hilo kati ya wakulima ambao ni jamii ya wagogo na wabena dhidi ya wafugaji jamii ya wamasai wengi wao wakitokea mikoa ya kaskazini yaani manyara na kiteto, hivyo basi kila jamii inajiona inamamlaka zaidi kuliko mwenzake.

Kwakuwa mgogoro huu bado haujapata utatuzi wa kudumu machafuko yamekuwa yakiendelea kila kukicha huku jamii kubwa inayo adhilika ni wakulima hasa kabila la wagogo, vifo hivyo vimekuwa vikitokea hasa kwa kabila la wagogo kwasababu mara nyingi wamekuwa vibarua walioajiliwa na watu wa jamii ya wabena hivyo katika kipindi chote cha kilimo huishi katika mashamba.

Jitihada kubwa Zimekuwa Zikifanywa na vingozi mbalimbali wakijaribu kutatua mgogoro huu akiwemo mbunge wa Dodoma mh. Jobu ndugai, japokuwa jitihada zake bado hazijaonesha mafanikio yoyote hadi sasa.


Mgogoro huu sio wa Ndugai peke yake au wakulima na wafugaji wa mkoa wa Dodoma tu, yatupasa jamii yote ya watanzania kushirikiana kwanguvu ili kushuluhisha mgogoro huu kama si kuumaliza kabisa kwakuwa hakuna kisicho wezekana endapo tutawekania dhabiti katika jamobo hili. 

Wakulima wakichangia jambo ka