Pages

Monday, 22 September 2014

KERO HII MPAKA LINI?



Kumekuwa na tatizo ambalo limekuwa likiwatesa abiria waendao mbezi kutoka kariakoo la kupigana vikumbo na wapiga debe wa kituo cha daladala cha karikoo madukani.


Pindi ifikapo muda wa mchana na jioni wananchi wamekuwa wakisumbuliwa na wapiga debe ambao wamekuwa na tabia ya kugombea siti za daladala kwa nia ya kuwalipisha abiria ndipo wapate kukaa kama sio hivyo watasimama.

jambo hili lilianza kitambo sana ila kwa sasa imekuwa kama ajira kwa wapiga debe wa kariakoo imefika wakati kila daladala inapofika hukimbilia kwa kasi utadhani wao ni wasafiri, na pia wamekuwa wakiwaibia baadhi ya abiria vitu mbalimbali ikiwemo mikoba, pesa, na simu za mkononi.

Kwa ujumla maisha ya wakazi wa mbezi yamekuwa magumu kwao kwani wamekuwa wakilipa nauli mara mbili zaidi ya ile iliyopangwa na SUMATRA. 


Baadhi ya makondokta wamekua chanzo kikuu cha kuwatoza abiria kiwango kikubwa cha pesa na tatizo hilo limepelekewa na kukatizwa kwa safari ilikupata  faida zaidi kwa manufaa yao binafsi.

Wapiga debe wamekuwa wakiwahia viti vya daladala kwaajili ya kupata ujira wa shilingi 500 mpaka 1000 na huwa wakali kama mbogo endapo wakikuachia nafasi ya kukaa halafu usiwape haki yao.

Kuna umuhimu mkubwa sana wa jamii na watu husika kulitambua jambo hili kama kero kubwa, lakini ni jambo la msingi kutatua hili tatizo kwa nia ya kuzuia baadhi ya matatizo kama ya kuibiwa pamoja na kupunguza gharama za maisha.   



kituo cha daladala kariakoo madukani.

  

No comments:

Post a Comment